Powered By Blogger

Karibu/Welcome

mambo?!

Sunday, January 11, 2009

Saikolojia Tanzania

Nasikitishwa na uchache wa wataalamu wa saikolojia nchini kwetu Tanzania. Hali ngumu ya maisha, matatizo mbalimbali ya kiafya, kielimu, na kimahusiano kwa ujumla husababisha watu wengi kuteseka na maradhi ya kiakili bila kueleweka na jamii wanamoishi. Matokeo yake ni kufanya maisha kuzidi kuwa magumu. Wakati mwingine jamani kupata mtu wa kumsikiliza shida za mtu tu huweza kuboresha hali ya mtu kwa kiwango kikubwa kabisa.

Binadamu wote hufikwa na majanga yanayo changanya akili wakati na wakati, sisi si miungu, tunahitaji misaada ya binadamu wenzetu...au hata wanyama wakati mwingine ili kuendelea kuishi katika hali nzuri kiakili. Wapo watoto wengi wanaouguza wazazi wao walioathirika na virusi vya ukimwi, kwa kweli huu ni mzigo mkubwa kwa watoto ambao bila ya msaada wa ndugu, jirani, jamaa huweza kuathiri maisha yao hata ukubwani. Wakati mwingine hata hao jamaa wanaweza wasisaidie katika kusaidia kuponya mioyo inayonung'unika ya watoto hao. Hapo ndipo msaada wa wataalamu wa saikolojia unapokuwa muhimu haswa.

Matatizo katika mahusiano kati ya binadamu na wenzake; iwe mpenzi, mzazi, rafiki, au hata mfanyakazi mwenziwe huweza kusababisha mtafaruku na mfarakano. Wapo watu wengi wenye akili mno ambao hufikwa na misukosuko ya mahusiano wasijue la kufanya, msaada wa mwanasaikolojia huweza kumsaidia kufikiri na kutatua tatizo alilonalo kwa ufasaha.

Tupo wengi tunaoishi ughaibuni, binadamu wote wana haki ya kutafuta maisha bora kuliko waliyo nayo, tena ikumbukwe kuwa tupo jinsi tulivyo kwa sababu ya kukimbia maumivu (kiroho, kiakili, kijamii, kifedha n.k) na kutafuta raha (raha ya moyoni). Wakati mwingine hutafuta raha kwa gharama ambayo mioyo yetu haiwezi kuibeba....matokeo yake tunajikuta tunaojiongezea lundo la maumivu tunayoyakimbia. Si rahisi kuishi mbali na watu wako, familia n.k. Wapo wanaoishi kwa uoga, wengine bila ya mapenzi ya kweli ndani ya nyumba...na hawana wa kumweleza masononeko ya nyoyo zao. Nipo kwa ajili yenu nyote (kadri ya uwezo wangu). Tafadhali usijikalie kimya kwenyekona huku ukiumia kila siku...msaada upo. Usiteseke bure, binadamu ni waovu sana....lakini ni wema mno.

Kama unatatizo lolote, swali, au chochote kile kinachosumbua roho yako na akili yako, tafadhali nitumie e-mail. Ukitaka weka jina lako, au nickname, au kuwa anonimous. Nitafurahi kukupa ushauri wangu, na endapo ni suala gumu kwangu...nitatafuta wenzangu tushirikiane. Swali lako litasaidia wengi zaidi, you will be paying it forward...just for your question. Ombi/swali lako pia ni msaada kwangu katika kuboresha taaluma hii ya saikolojia ya ushauri....na itanisaidia kuwa na uzoefu zaidi na uwezo zaidi wa kusaidia wengine.

Tuma swali, ombi maoni kwangu kwa lugha ya kiswahili, au English. Ninatumia kiswahili ili wengi walio nchini Tanzania wasioelewa vizuri lugha ya kiingereza waweze kufaidika. Lakini nitakuwa nikibadilisha badilisha au hata kuchanganya...napenda ujisikie huru kufanya hivyo pia.

Dr. Wannabe
e-mail (wannabe.dr@gmail.com)

2 comments:

Anonymous said...

Dr.Wannabe
Mi nataka makalatasi....huk za sista up!, si unasaidia watu?

Anonymous said...

Ndugu yangu mtanzania mwenzangu kabla sijasoma maelezo yote hapo chini naomba kwanza kabisa nikupongezi kwa jambo hili. Mimi binafsi nimekuwa natatizwa sana na swala hili la nchi yetu kukosa wataalamu wa saikolojia kwani naelewa umuhimu wao na jinsi gani wanaweza kutusaidia kututibu kiakili. Mimi mara nyingi nimekuwa na matatizo ambayo nahitaji mtu atakaye nisaidia kisaikolojia lkn nimekuwa nagonga mwamba. Unajua tuna wakubwa ambao unaweza kuwaomba ushauri lkn hawana utaalamu wa kutosha, ama wakati mwingine unaweza kuishia kumueleza rafiki yako wa karibu matatizo yako matokeo yake anaenda kukutangazia kwingine. Kwakweli mimi nakupongeza sana kwa hili na naomba mjitahidi sana kuwaelimisha watanzania juu ya jambo hili kwani wengi hawaamini kama inasaidia hivyo mna kazi mbili hapo. Mimi mwenyewe as i speak nina mengi sana ninayohitaji ufumbuzi natafuta mda mzuri nitulie nitakuandikia utakapo nijibu najua maswali yangu mengi yatajibika and i will be in a good position to make my desicions.

Thanks alot keep up the good job.

Mdau